Saturday, January 17, 2015

SSERUNKUMA AANZA KUNGARA, YANGA WALAZIMISHWA SARE




Mfungaji bora wa ligi kuu ya Kenya (KPL) Danny Sserunkuma amefunga goli lake la kwanza katika ligi kuu ya vodacom ya Tanzania bara pale timu yake ya Simba SC ilipoibuka na ushidndi wa goli 2-0 mbele ya Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Katika mchezo huo Simba SC iliwabidi wangoje mpaka daika ya 32 kuandika goli lao la kwanza kupitia kwa Danny Sserukuma goli lililodumu mpaka mapumziko.


Katika kipindi cha pili Simba SC ambao walikuwa wameshinda mchezo mmoja wa ligi kuu ya vodacom na kutoka sare michezo 6 na kufungwa mmoja waliandika goli la pili katika dakika ya 62 kupitia kwa Elias Maguli.

No comments:

Post a Comment