KAMA ni mmoja kati ya watu waliojiunga na mitandao ya kijamii, kuna kitu ambacho aliandika jana Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe, ilikuwa ishu ya fedha ambayo tayari TRA imeanza kupata kutoka kwa wasanii wa Tanzania, Zitto kabwe ameongea na 255 na hivi ndivyo alivyofunguka;- Zitto Kabwe anasema "kuanzia mwaka 2012 tulikuwa kwenye kampeni kubwa ya kutaka kazi za wasanii zilasimishwa na tumefanikiwa kubadilisha sheria ya Ushuru wa Forodha na kuongeza kifungu kingine kinachotaka kuwepo stemp za kodi kwenye kazi za wasanii. Kutokana na utaratibu huo tangu uanze kwa miaka miwili TRA ilikusanya milioni 348 kutokana na kazi milioni 8 za wasanii ambazo zimesajiliwa". Kwa upande wa miito ya simu Mh Zitto Kabwe aliendelea kusema kwamba jana walijadili suala hilo, wataanza kukusanya kodi na kusimimia lengo likiwa kujua na kurekodi kiasi gani msanii analipwa na makampuni ya simu ili asilaliwe.
No comments:
Post a Comment