Thursday, January 22, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA - DIRISHA DOGO LA USAJILI

Chelsea wameanza mazungumzo na Fiorentina kuhusiana na kumnunua winga kutoka Colombia Juan Cuadrado, 26, mwezi huu (Guardian), Chelsea wameongeza juhudi zao za kumsajili Cuadrado baada ya dau lao la pauni milioni 20.6 kukataliwa na Fiorentina siku ya Jumatano (Times), Chelsea watamuuza winga Mohammed Salah, 22 au Andre Schurrle, 24 ili kuandaa kuwasili kwa Cuadrado (Independent), Schurrle anajiandaa kurejea Ujerumani na kujiunga na Wolfsburg (Daily Express), hata hivyo kocha wa Fiorentina Vicenzo Montella amesema Cuadrado haendi Stamford Bridge (Goal.com), Chelsea pia wanapanga kutoa pauni milioni 40 kumnunua kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba, 21 anayechezea Juventus,
 na ambaye aliondoka Man Utd mwaka 2012 kwa uhamisho wa bure (Daily Express), Valencia huenda wakawazidi kete Liverpool kwa kumsajili kiungo wa Manchester City James Milner, 29 (Daily Mirror), Manchester United hawajapata dau hata moja 


kumuulizia kiungo wao kutoka Brazil Anderson, 26 ambaye anauzwa na hajacheza tangu mwezi Agosti (Daily Mail), Manchester United wameanza mazungumzo na mshambuliaji kutoka Paraguay Sergio Diaz, 16 anayechezea Cerro Porteno (Tuttomercatoweb) Swansea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Blackburn Jordan Rhodes, 24 ili kuziba pengo la Wilfried Bony aliyejiunga na Man City (Daily Telegraph), QPR wanataka kumsajili Dani Osvaldo, 29 ili awasaidie kutoteremka daraja (Daily Mirror), mshambuliaji wa West Brom Georgios Samaras, 29 anajiandaa kujiunga na klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia kwa mkopo wa miezi sita (Express na Star) Arsenal watakabiliwa na ushindani kutoka Manchester United kumsajili beki wa kati wa Villarreal Gabriel Paulista ambaye ana thamani ya pauni milioni 16 (London Evening Standard). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!

No comments:

Post a Comment