Goli la mshambuliaji wazamani wa Simba SC Danny Mrwanda limeitosha kuipandisha Yanga SC kutoka nafasi ya 4 mpaka nafasi 2 wwakifikisha point 18 nyuma kwa point 2 toka kwa vinara Azam FC.
Yanga SC leo walikuwa wageni wa polisi Morogoro katika uwanja wa Jamhuri katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya vodacom ambapo itaendelela kesho kwa michezo 6.
Katika mchezo huo wa leo kama sio jitihada ya kipa wa Polisi M0orogoro Tom Kavishe Yanga wangeibuka na ushindi mnono hii leo, ambapo kipa huyo ametoa hatari nyingi golini mwake huku washambuliaji wa yanga wakipoteza nafasi mbili wakiwa na nyavu.
Yanga waliandika goli lao pekee katika dakika ya 42 ya mchezo kupitia kwa Mrwanda akimalizia mpira uliotemwa na kipa Tom Kavishe kufuatia mpira wa Saimon Msuva aliyeunga krosi ya Juma Abdul.
Polisi Morogoro hawakuwa nyuma katika kutengeneza nafasi kama Selemani Kassim Selembe angekuwa makini katika dakika ya 52 angeisawazishia Polisi Morogoro kuvuatia shuti lake hafifu kudakwa na kipa Ally Mustafa.
Na mwishoni mwa kipindi cha kwanza amanusura Polisi Morogoro kupata goli kama si umakini wa Juma Abdul aliokowa mpira karibu na mstari na mchezo kumalizika kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na kufikisha point 18.
No comments:
Post a Comment