Thursday, January 22, 2015

TUNDA - MAN BILA CHIDI BENZI NINGEKUA NIMEKUFA KIMUZIKI SOMA HAPA MCHONGO MZIMA


Bila chid Benzi Nisingefika Hapa na Kujulikana Kimuziki - Tunda Man Afunguka ya Moyoni
Msaniii Tunda Man ambae kwa sasa anatamba na hits song mbili Achana na mimi na Mapenzi yale yale amefunguka na kuweka wazi kuwa bila support kubwa ya msanii Chid Benzi huenda asingekuwepo katika tasnia ya muziki kwa sasa. Mkali huyo Tunda Man

ambaye alianza kutamba na wimbo wake wa Neila ambao alimpa shavu Chid Benz amefunguka hayo katika ukurasa wake wa Instragram.
Tunda alisema kuwa verse aliyochana Chid Benz katika wimbo wake wa kwanza ndiyo uliweza kumfanya asimame vizuri katika tasnia ya bongo fleva

"Yes verse ya neila ilikuwa kali sana ndio imenitambulisha kwenye ulimwengu wa music" hivyo huwa na heshimu sanaa mchango wake katika kazi zangu na ndiyo maana siku zote namkubali na kumheshimu Chid Benz maana ndiyo alinifanya nisimame na kufanya vyema katika muziki.

"I think without Chid Benz i could not be where I'm now that means he contribute a very big percent of occupation in this game. That's da reason why i do appreciate this nigger"
Msanii Chid Benz ambae kwa sasa anakabiliwa na kesi ya kukamatwa na madawa ya kulevya katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere,kabla ya kuanza kutumia madawa ya kulevya msanii huyo alikuwa mfano wa kuigwa na alikuwa msaada mkubwa kwa wasanii mbalimbali kwa kuweza kufanya kazi nyingi kwa lengo la kuwapa msaada wasaniii wachanga ambao waliweza kupenya na kufanya poa pindi walipomshirikisha mkali huyo.

No comments:

Post a Comment