Jiji la
dar es salaam huwa ni tamu lakini lina kero zake na
uenda kero ni nyingi kuliko raha zilizopo… moja wapo ya
kero kubwa zaidi ni hili ambalo bila shaka kila mmoja
wetu anayeishi uswahilini linamgusa kwa namna moja
ama nyingine … si linguine ni swala hili la miziki ya
kukesha ambayo imejichukulia umaarufu kwa jina la
vigodoro, kwa mtu anaye kaa mitaaa ya mbezi beach,
upanga au masaki ni vigumu kuelewa nachomaanisha
lakini kwa watu wa yombo vituka, tandale kwa tumbo ,
ukonga mazizini na sehemu kama tandika wananielewa
vizuri…
Ni ukweli usiopingika kuwa hii ni kelo ya watanzania
wengi hapa jijini, mara nyingi miziki hii uanza siku ya
alhamisi au ijumaa na kwenda mpaka jumapili… kero hii
inatokana na mtindo wa upigaji wa mziki huu usiozingatia
mda ambapo upigwa mpaka asubuhi bila kujali usumbufu
mkubwa wanoupata watu wa karibu na vigodoro hivyo…
sasa pata picha umerudi toka kazini sa tano usiku
kutokana na foleni iliyopo mjini na unaamua kujipumzisha
kidogo ili uwahi kuamka ukatafute riziki… kwa sauti ya
mziki huu sidhani kama utapata usingizi … kitu ambacho
kinaweza kupelekea uamke umechoka na ushindwe
kufanya kazi zako kwa ufasaha,,,, hapa tunaweza kusema
kwamba miziki hii inarudisha nyuma maendeleo ya
watanzania nan chi kwa ujumla. Kero nyingine ya miziki
hii ya usiku ni ukiukwaji wa maadili ya mtanzania kwani
kubali ukatae watu wanacheza bila kuhofia chochote na
mara nyingi kama unavyojua nyumba zetu za uswahilini
wengi hatuna mageti ya kuwazuia watoto wetu… watoto
wengi wa umri wa chini ya miaka kumi na nane
wamekuwa wakitoroka nyumbani na kukimbilia kwenye
vigodoro hivo na kuwafanya wajifunze tabia ambazo ni
zaidi ya umri wao.
Nadhani imefika wakati sasa serikali kuangalia upya
sharia za upigaji mziki katika kumbi za starehe na
majumbani.. mara nyingi sharia inasema baa zifungwe sa
sita labda uwe na kibali naalum kutoka sehemu husika ..
lakini hii imekua ni tofauti kwa vigodoro kwani uenda
mpaka asubuhi na kusababisha kero isiyokuwa ya
kawaida kwa wakazi wa maeneo ya uswahilini
No comments:
Post a Comment