MAKAMU wa Rais ,Dk.Mohammed Gharib Bilal anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Jumamosi Januari 17 katika Kijiji cha Kiromo, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mikocheni Dar es Salaam, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia Fedha na Utawala, Dk.Elifuraha Mtalo alisema sherehe hizo zitafanyika Katika Kijiji cha Kiromo na kwamba uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao unatarajiwa kuanza Mwaka huu.
Dk.Mtalo alisema Dk.Bilal ndiye atakuwa mgeni rasmi pia na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa naye anatarajiwa kuwa miongoni mwa wageni walioalikwa katika sherehe hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu Somo la Historia linatufundisha kuwa mji wa Bagamoyo watumwa walikuwa wakiishi.
" UB tunaifahamu historia ya Mji wa Bagamoyo ndiyo maana tukaamua kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la University of Bagamoyo.Kupitia Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, hivyo kupitia UB ambayo inajenga makazi yake ya kudumu katika mji huo, binadamu wote watakuwa huru kwasababu tutapata elimu" alisema Dk.Mtalo.
Alisema UB ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya muda ,Mikocheni B, Dar es Salaam na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu ya UB kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu na ajira.
Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo
No comments:
Post a Comment