Nchi ya Ubelgiji ilipitisha sheria ya watu wanaotaka kufa kusaidiwa kwa kudungwa sindano kwa miaka 12 iliyopita.
Frank Van den Bleeken aliwasilisha ombi lake kwa Serikali ya nchi hiyo kwamba asaidiwe kufa kwa kudungwa sindano yenye sumu ili kumwepushia msongo wa mawazo anaokabiliwa nao kutokana na kukabiliwa na kesi ya mauaji na ubakaji.
Kwa miaka mingi mtuhumiwa huyo alisema kuwa alishindwa kabisa kubadili au kukomesha tabia yake ya ubakaji na kutokana na hilo haoni uwezekano wowote wa kuachiwa huru hivyo aliomba kuchomwa sindano ili apoteze maisha.
No comments:
Post a Comment