Tuesday, January 13, 2015

WABUNGE WAAMUA MISHAHARA YAO IPUNGUZWE



Wabunge wa bunge la Burkina Faso wamekubali kupunguza mishahara yao kwa asilimia hamsini.

Uamuzi wa Wabunge hao unatokana na kuibuka kwa malalamiko ya wananchi katika mitandao ya kijamii nchini humo kuwa wamekua wakipokea kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya milioni nne kwa mwezi huku mfanyakazi wa kawaida akipokea dola moja na nusu.
Mshahara huo unajumuisha marupurupu ya kuhudhuria vikao vya bunge, kulipia ofisi, bima ya afya pamoja na fedha za kununua Petrol.

No comments:

Post a Comment