Jina lake halisi anaitwa Brian Deacon, amezaliwa February 13, 1949 huko Oxford, United Kingdom (Uingereza). Brian alipata elimu ya msingi na sekondari katika shule za kisasa hadi alipofikisha umri wa miaka 17. Baada ya hapo alifanya kazi ya usafishaji madirisha na dereva wa gari ya bucha wakati huo akiwa mwanachama wa Oxford Youth Theatre (kundi la sanaa la vijana wa Oxford). Kazi anayoifanya hadi sasa ni sanaa ya uigizaji ambayo ameianza rasmi tangu mnamo mwaka 1971 kipindi hicho akiwa na umri wa miaka 22 tu.
Mnamo mwaka wa 1976 na 1978, Brian aliigiza kwenye mchezo maarufu kwa jina la "The Feathered Serpent" au "Nyoka mwenye Manyoya" (kwa lugha ya Kiswahili); ambae katika maigizo hayo Brian aliigiza kamaa "Heumac".
Katika mwaka wa 1979, Brian alipata fursa ya kuigiza kupitia shirika la Uinjilisti lililojulikana kwa jina la the Jesus Film Project; wakati huo Brian alikuwa na umri wa miaka 30, alishiriki kwenye usaili wa kutafuta mwigizaji atakayeigiza kama Yesu kwenye filamu walioipa jina la "JESUS". Waigizaji zaidi ya watu elfu moja waliingia kwenye kinyang'anyiro hicho, lakini walichujwa hadi kubaki waigizaji 260 ambao walifanyiwa majaribio ya kuigiza ili kumtafuta anayefaa kuigiza kama Yesu kwenye filamu hiyo; alikuwa mwigizaji pekee kutokea Uingereza kati ya Waisraeli wengi walioingia kwenye mchujo huo. Jambo la kustaajabisha; mwigizaji Brian Beacon alifaulu kuigiza vizuri zaidi ya wenzake, jambo hilo lilimfanya ateuliwe kuigiza kama Yesu katika hiyo filamu iliyopewa jina la "JESUS" mnamo mwaka wa 1979. Katika usaili huo hawakuzingatia kigezo cha utaifa, wala hawakutafuta mtu mwenye sura ya kufanana na Yesu (kwa maana hapa duniani hakuna mtu anayeijua sura halisia ya Yesu wala picha ya Yesu), bali walizingatia kigezo cha mtu ye yote yule atakayeigiza vizuri tu.
Kisha, Brian Deacon aliigiza kama Yesu kwenye filamu hiyo waliyoicheza huko Israel mnamo mwaka huo wa 1979, filamu ambayo imemfanya Brian kuwa maarufu sana kiasi kwamba hata baadhi ya watu hutumia picha zake kwa kuzipamba sehemu mbalimbali na baadhi yao wanaamini kabisa kuwa picha hizo ni sura halisi ya Yesu, kitu ambacho sio kweli hata kidogo.
Historia kwa ufupi:
Asili ya kuigizwa filamu hiyo inatokana mnamo mwaka 1945 wakati mfanyabiashara kijana mmoja jina lake Bill Bright alipotaka yeye binafsi kufadhili fedha kwa ajili ya kuigiza filamu inayohusu maisha ya Yesu Kristo, ambayo itakuwa na mvuto, iwe sahihi Kibiblia, na ambayo inaweza kutafsriwa katika lugha tofauti tofauti mbali na Kiingereza tu.
Badala ya kufanya filamu kwa wakati huo, Bill Bright alikwenda kutafuta huduma ya Kikristo, akapeleka wazo lake kwa wanafunzi wa chuo kinachoitwa Campus Crusade for Christ mnamo mwaka 1951. Mwaka wa 1976 ushawishi wa Campus Crusade ulizidi kuenea zaidi ya maeneo ya chuo, sokoni na sehemu mbalimbali katika jamii; ndipo Bill Bright akatilia upya umaanani kuhusu kurekodi maigizo (filamu) inayohusu maisha ya Yesu. Ndipo mwandaaji wa filamu kutoka Hollywood, Mjerumani aitwaye John Heyman alimwendea Bill Bright kumwomba ufadhili kwenye mradi wa kuigiza Biblia yote na kuiweka katika filamu. Lakini mradi huo baadae ulifanywa kwa kutumia kitabu kimoja tu cha Injili ya Luka katika Biblia.
Filamu hiyo waliyoipa jina la "JESUS", iliongozwa (directed by) na Peter Sykes, John Krish, pamoja na John Heyman; Wazalishaji (Producers) walikuwa: John Heyman pamoja na Richard F. Dalton; Aliyeiandika (Writter by) ni: Barnet Bain kwa kutumia kitabu cha Injili ya Luka; Nyota (Starring) wa filamu hiyo ni Brian Deacon aliyeigiza kama Yesu; Sehemu ya Mariamu mama wa Yesu iliigizwa na Rivka Neumann; Sehemu ya Yesufu iliigizwa na Yosef Shiloach; na sehemu ya Mariamu Magdalena iliigizwa na Talia Shapira; Filamu hiyo imesimuliwa (Narrated by) na: Alexander Scourby; Muziki umeingizwa na Nachium Heiman; Imesambazwa (Distributed by) na: Inspirational Films (Warner Bros); Imetolewa rasmi mnamo tarehe 19 Oktoba 1979 huko Marekani; Filamu hiyo inatumia muda wa dakika 115 tu. Maeneo yaliyotumika kuigiza filamu hiyo ni Mashariki ya Kati; Filamu hiyo iliigizwa awali kwa lugha ya Kiingereza; na hadi kukamilika, filamu hiyo ilitumia bajeti ya kiasi cha dola za Kimarekani milioni sita (6). Ilitumia hadi miezi 18 mpaka kukamilisha kazi nzima ya kurekodi maigizo hayo; ikawa ni filamu ya kwanza kihistoria kutengenezwa inayohusu maisha ya Yesu.
Filamu hiyo imetokea kufanya vizuri katika sanaa ya uigizaji na kufanikiwa kutazamwa na mamilioni ya watu duniani kote, pia imetafasiriwa kwa lugha mbalimbali zaidi ya 1,000 na zaidi ya lugha 235 bado sasa zipo kwenye zoezi la kuifafasiri kiasi kwamba filamu hiyo imevunja rekodi ya kutafasiriwa kwa lugha nyingi. Inawezekana lengo la filamu hiyo ni kuifikisha Injili kwa njia ya maigizo ili watu waone mfano wa jinsi Yesu alivyofanya huduma Yake hapa duniani, lakini watu wengi wameipokea kwa hisia tofauti hadi kuwafanya kuamini kuwa huyo ni Yesu Mwenyewe!
Nakepnda kusisitiza kwamba: HUYU SIO YESU, BALI NI MWIGIZAJI TU ! Hayo ni maigizo tu.Filamu hiyo hutumika katika mikutano mingi ya Injili na kuwafanya watu wengi kuokoka; na kweli imechangia kwa kiasi kikubwa watu kuelewa maisha ya Yesu na mfano wa jinsi alivyoteswa; na watu wengi wameokoka kupitia Injili hiyo iliyofanywa kwa namna ya maigizo.
Nimeguswa kufundisha somo hili kwa sababu watu wengi wamepotoshwa na kuaminishwa vibaya kuwa sura hiyo ni ya Yesu, kitu ambacho ni ubatili mtupu. Ninaamini Brian hakuigiza ili watu wamwite yeye Yesu, lakini nia yake ilikuwa ni kuigiza tu ili alipwe pesa, kwa maana aliajiriwa na alifanyiwa usahili kwa ajili ya kuigiza hivyo; na pia lengo la waandaaji wa filamu hiyo (Jesus Film Project) walikuwa na lengo tu kufanya mahubiri kwa njia ya uigizaji tu.
Mbali ya kuigiza filamu hiyo (JESUS), Brian aliendelea na sanaa yake ya uigizaji ambapo mnamo mwaka wa 1985 alionekana katika Peter Greenaway film, iliyopewa jina la "A Zed & Two Noughts", kwenye filamu hiyo, Deacon aliigiza kama Oswald Deuce, na miongoni mwa waigizaji katika filamu hiyo yumo pia kaka yake ajulikanae kwa jina la Eric Deacon.
Maisha yake binafsi tofauti na sanaa:
Brian Deacon ameingia katika ndoa mara mbili; ndoa yake ya kwanza ni kati yake na Rula Lenska ambayo ilidumu tangu mnamo mwaka 1977 hadi 1987, katika ndoa hiyo alipata kumzaa binti aliyempa jina la Lara Deacon. Ndoa yake ya pili aliifunga na Natalie Bloch mnamo mwaka 1998, ndoa hiyo inaendelea hata sasa.
Huyu ndiye Brian Decoan mwigizaji aliyecheza kwa jina la usanii la "Jesus" katika filamu iliyopewa jina "JESUS" mnamo mwaka 1979, na hiyo ni historia fupi kumhusu yeye pamoja na filamu ijulikanayo kwa jina la 'JESUS"
Amezaliwa February 13, 1949 huko Oxford, United Kingdom (Uingereza) kutoka kwenye familia ambayo mama yake ni Mkatoliki wakati baba yake ni Mprotestanti.Hadi mwaka huu 2014, Brian anaumri wa miaka 65.
KUHUSU MATUMIZI YA PICHA NA MICHORO KWA KUIFANANISHA NA YESU:
Kwa mtazamo wa nje jambo hilo linaonekana jema linalowasaidia watu kufundisha kwa mifano; lakini, kwa upande mwingine jambo hilo limechangia kupotosha watu wengi na kuwaingiza katika kumkufuru Mungu!
Hata kabla ya kuchezwa filamu hiyo maarufu kwa jina "JESUS", kwa karne nyingi zilizopita hao wapagani wamekuwa wakitumia picha na sanamu ambazo wanadai huzitumia kama vielelezo vya kufundishia.
Hapa naongelea picha za kuchorwa ambazo watu wasio na ufahamu hizidhania kuwa ndiye Yesu; baadhi ya picha hizo zinayo maneno yaliyoandikwa namna hii: "Huyu Ndiye Mwokozi wa ulimwengu", au "Bwana Yesu ilinde familia hii", n.k; kisha wamebandika picha hizo katika kuta zao na sehemu mbali mbali hata katika nyumba za ibada na katika vitabu vya mafundisho ya dini zao. Kwa kweli maneno hayo katika picha hizo hayampi utukufu Mungu, kwa maana kiuhalisia picha hizo sio za Yesu.
Watu wengi wameaminishwa hivyo; ndio maana watu wengi waonapo picha hizo hata kama haijaandikwa cho chote, ukiwauliza: "Huyo ni nani?", utasikia wakikujibu: "Huyo ni Yesu". Sipingani na kukua kwa sayansi na teknolojia, lakini nasisitiza tu; hayo maigizo yaelezwe kwa watu kwa uwazi watambue kuwa hao ni waigizaji tu; pia hizo picha hazifai kuandikwa: "Huyu Ndiye Mwokozi wa ulimwengu", kwa kufanya hivyo ni sawa na kumkufuru Mungu.
Kuna usemi mmoja wa usemao: Ukisikia / ukiona vibaya, utajifunza vibaya; ukijifunza vibaya, utaamini vibaya; ukiamini vibaya, utatenda vibaya!
Kwa kweli, sio sahihi kutumia picha hizo katika ibada, na pia sio sahihi kutumia picha yo yote kuifananisha na Yesu. Biblia inatuambia kwamba Yesu ni Mungu aliyejidhihirisha katika mwili:
Yesu ni Mungu aliyeuvaa mwili, kwa hiyo sio sahihi kuchora picha ya ubunifu ambayo sio sura halisi ya Yesu alafu ukaifananisha na Yeye. Ifahamike tu kwamba: picha hizo sio sura ya Yesu; hayo ni maigizo tu, na hiyo ni michoro tu, na itabaki kuwa michoro tu! HUYO SIO YESU !"Na Bila shaka siri ya utauwa ni kuu, Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na Malaika, akahubiriwa katika mataifa, akaaminiwa katika ulimwengu, akachukuliwa juu katika utukufu," ~ 1 Timotheo 3:16
You might also like: FILAMU YA SIKU YA MWISHO KUTOKA WIKI HII-666 FIMALU YA DUNIA HAINA HURUMA KUANZA KARIBUNI Linkwithin Posted by Musa Shigela at 1:01 PM Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Newer Post Older Post Home Subscribe to: Post Comments (Atom) POSTED TITLE Related Posts Plugin for WordPress, Blogger... TANZANIA ONE - MUSA MATEJA View my complete profile Search
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
You might also like: FILAMU YA SIKU YA MWISHO KUTOKA WIKI HII-666 FIMALU YA DUNIA HAINA HURUMA KUANZA KARIBUNI Linkwithin Posted by Musa Shigela at 1:01 PM Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Newer Post Older Post Home Subscribe to: Post Comments (Atom) POSTED TITLE Related Posts Plugin for WordPress, Blogger... TANZANIA ONE - MUSA MATEJA View my complete profile Search
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
No comments:
Post a Comment