Tuesday, January 13, 2015

iOS8 SIMU YA UKWELI TOLEO JIPYA HII HAPA

habari njema kwa watumiaji wa vifaa vya apple. iOS 8 imetoka, ila sio habari njema kwa watumiaji wa vifaa vya apple vya zamani kama original iPhone, iPhone 3G, 3GS au 4, mna bahati mbaya. Wenye iPhone 4s, 5, 5c na 5s wataweza ku install iOS 8, pia wenye  iPod Touch ya kizazi cha tano.

KUNA MAPYA YAPI KWENYE iOS 8?

  • iMESSAGE. Sasa ivi unaweza kushea sauti yako kwa kutap na kutuma sauti. Apple imerahisisha utumaji wa picha na videos. Kwenye group messages unaweza kuchagua kuwatoa watu ambao hutaki wasome izo message, au unaweza kuchagua usitumiwe izo message. Unaweza kushea location kwenye message unazotuma.
  • PICHA kwenye iOS 8, sasa kuedit picha kumerahisishwa zaidi, Apple wameiongezea vikorombwezo app ya Photos ambapo imekuwa rahisi zaidi kubadili exposure, brightness, contrast, highlights, shadows na zaidi.
  • QUICKTYPE utabiri wa maneno wakati ukitype kwa kutumia keyboard ya Apple QuickType umekuwa wa kijanja zaidi, ukio binafsi zaidi na wakuvutia. Inaweza kubashiri kuwa sasa una type na itakuletea maneno au vifungu vya maneno aambavyo inadhani unataka kuandika, ikikumbuka maneno uliyotumia kabla katika message zilizopita. QuickType inaelewa unavyowasiliana na, inaweza kukushauri maneno unayopenda kuyatumia mara kwa mara, kwa iyo unaweza andika sentesi ndeeefu kwa kugusa mara kadhaa tu.

  • HEALTHKIT hii ni aplikesheni mpya ambayo itakuwa ikikusanya taarifa zote za afya kutoka application zako zingine za afya na kuziweka pamoja, pia itaweza kufanya kazi pamoja na apple watch kipindi itakapotoka, ambapo itaweza kukusanya taarifa zako za mapigo ya moyo na kadhalika


  • FAMILY SHARING hii itaweza kuwasiliana na vifaa vingine vya wanafamilia ambapo utaweza kushea vitu gani umefanya manunuzi na wanafamilia wako, pia unaweza shea nyimbo zako, videos, picha hata vitabu na wanafamilia wengine ambao umewaunganisha pamoja nawewe.
  • CONTINUITY  Labda tuseme simu yako ya iPhone imezimika kabla hujamaliza kutuma barua pepe yako, au kusoma ujumbe,  basi hii application inakuruhusu vifaa vyako kama iPad, iMac na MacBook viwasiliane na simu yako ili mradi viwe karibu karibu na utaweza kuendelea kusoma pale ulipoishia, is that cool?
  • iCLOUD DRIVE hii application itakuwezesha kuhifadhi mafaili yako, iwe picha, videos au mafaili mengine, pia itakuwezesha kuyahariri bila kujali unatumia mfumo gani kiwe kifaa kinachotumia iOS, Mac, Windows PC au kupitia www.icloud.com.

No comments:

Post a Comment